Mahakama yalinda marupurupu na haki za kisiasa za marais wastaafu

By Citizen TV Kenya

Community Score: 50% | 41 views | 3w

0 community ratings: null thumbs up, null thumbs down

Mahakama Kuu imebatilisha baadhi ya vifungu vya Sheria vya marupurupu ya Marais Wanaostaafu kuwa kinyume na Katiba. Katika uamuzi WA Jaji Bahati Mwamuye, amesema vifungu vya 4(1), 4(2) na 4(3) vya Sheria ya marupurupu ya Marais Wastaafu haviwezi kutumiwa kupunguza, kunyima, kuzuia, kuondoa ama kubadilisha kwa hasara marupurupu anayostahili Rais mstaafu. Mahakama pia imetangaza Kifungu cha 6 cha Sheria ya Mafao ya Marais Wastaafu kuwa kinyume na Katiba na kukibatilisha kwa ujumla. Kifungu hicho kilikuwa kinaweka vikwazo kwa Rais mstaafu kushiriki kikamilifu katika siasa. Kwa mujibu wa Mahakama, vikwazo hivyo haviendani na haki za kisiasa zinazolindwa na Katiba.

Tags: Citizen TV, Citizen TV Live, Livestream, News

More from Citizen TV Kenya

  • | DAY BREAK | Finance bill 2026 explained [ part 1] — Score: 50%
  • The explainer interview | Day of delayed justice — Score: 50%
  • THE EXPLAINER 23RD JUNE, 2026 — Score: 50%
  • KNCCI launches youth enterprise program — Score: 50%
  • Family Bank debuts on NSE in major market listing — Score: 50%
  • Teen girl hospitalized after assault as another family seeks justice in Thika murder — Score: 50%