Kisa cha kwanza cha Ebola chathibitishwa Kenya
Community Score: 50% | 106 views | 1w
0 community ratings: null thumbs up, null thumbs down
Mkenya wa kwanza kutambuliwa kuwa na ugonjwa Ebola hapa nchini ameaga dunia. Mgonjwa huyo aliyewasili kutoka DRC na kupitia Uganda kabla ya kuwasili nchini, alichukuliwa na jamaa zake kutoka uwanja wa ndege wa JKIA na kupelekwa kwa matibabu baada ya kuonyesha dalili za ugonjwa Ebola. Waziri wa afya Aden Duale ambaye ametoa taarifa hiyo leo anasema mgonjwa huyo alifariki wakati akiendelea kupokea matibabu katika karantini. Alikuwa akifanya kazi nchini DRC. Kulingana na Duale, jamaa za muathiriwa huyo ambaye walitangamana naye baada ya kuwasili nchini wametambuliwa na wamewekwa karatini kwa siku ishirini na moja. Abiria waliokuwa naye kwenye ndege pia wanatafutwa ili kutambuliwa na kupewa huduma zifaazo.
Tags: Citizen TV, Citizen TV Live, Livestream, News
More from Citizen TV Kenya
- | DAY BREAK | Finance bill 2026 explained [ part 1] — Score: 50%
- The explainer interview | Day of delayed justice — Score: 50%
- THE EXPLAINER 23RD JUNE, 2026 — Score: 50%
- KNCCI launches youth enterprise program — Score: 50%
- Family Bank debuts on NSE in major market listing — Score: 50%
- Teen girl hospitalized after assault as another family seeks justice in Thika murder — Score: 50%